0

Mrembo wa Burma mwenye umri wa miaka 16, May Myat Noe amegoma kurudisha taji la Miss Asia Pacific World Pageant hadi pale waandaaji wa shindano hilo watakapomuomba radhi kwa kumuita muongo na mwizi.
Kwa mujibu wa Telegraph, mrembo huyo ambayo ndiye msichana wa kwanza kutoka Burma kushinda taji hilo la kimataifa anadai kuwa mwakilishi wa kampuni hiyo aliongopa kuhusu umri wake wakidai kuwa alikuwa na miaka 18 badala ya 16 na kwamba walikuwa wanamlazimisha kufanya upasuaji (plastic surgery) kutoka kichwani hadi kwenye kidole gumba.
Noe huyo huyo ameeleza kuwa hataki kingine zaidi ya kuombwa radhi kupitia vyombo vya habari kama walivyofanya wakati wa kumchafua.
“Sijivunii hata kidogo kuwa na taji hilo, sitaki taji kutoka kampuni ambayo ina sifa mbaya.” Amesema Miss Myat Noe.
Taji hilo limetajwa kuwa na thamani ya kati ya $100,000 (zaidi ya Milioni 166 za Tanzania) na $200,000.

Post a Comment

 
Top