Nice ambaye ni mwimbaji na mwanzilishi wa staili ya Takeu, amesema amefanya kazi mpya na producer wake wa kwanza aliyemtoa aitwaye Kameta.
“Napenda kuwajulisha marafiki zangu wote wa Tanzania, wapenda muziki kwamba nimefanya na rafiki yangu wa zamani Kameta producer ambaye ndio wa kwanza kufanya kazi na mimi”.Mr Nice aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
“Kilichokuja kunikwamisha ni baada ya kupata ajali kwasababu unajua niliumia sana kama ulisikia niliokuwepo nao wote walikufa mi nikabahatika kusalia mwenyewe tu ikawa kidogo imeniweka chini, unajua maswala ya kuvunjika ukishavunjikavunjika tena sio kitu cha siku mbili tatu.” Amesema Nice.
Nice ameongeza kuwa kabla mwaka huu haujaisha tayari atakuwa ametoa kazi hiyo mpya sababu anajipanga kufanya na video.
“Kabla ya mwezi desemba nitakuwa na kitu ambacho ni very special ambacho nimewawish wanawake wote wa Tanzania na dunia nzima, lakini kwa sasa hivi nipo katika final recovery ya tangu nipate ajali.”
Kameta ndiye producer aliyemtoa mr Nice na kumtengenezea album yake ya kwanza iliyokuwa na hits kama ‘Kikulacho’, ‘Kidalipo’ na zingine.
Post a Comment