0
Miongoni mwa ndoto alizonazo kila msanii ni pamoja na kuwa mwanamuziki mkubwa wa ndani na baadae kuvuka mipaka ya nyumbani na kutambulika nje. Roma amekiri kuwa miongoni mwa wasanii wenye ndoto hizo japo amekosa jibu la kwanini mpaka sasa hajaanza kupata mashavu kama ya Diamond ya kupata show za nje.
roma
Kupitia Instagram rapper huyo amezungumza na msahabiki wake kwa kuwauliza maswali ya kwanini hajaanza kuitwa kwenda kutumbuiza nje ya nchi.
Hiki ndicho alichokiandika juu ya picha aliyopiga akiwa uwanja wa ndege.
“Hivi #mashabiki zangu niwaulizeni #kitu!!! Hivi ni kweli kuwa wale #wabongo wanaoishi #nchiZaNje Kama #Germany#U.K#USA#S.A#SWEEDEN#NORWAY# na kwingineko Hivi nikiwaimbia #KKK#MAUMIVU#2030#KIDOLECHAMWISHOJUU#MATHEMATICS hivi hawataruka na kuenjoy Show!!??? Sasa mbona simu haziiti???
Unajua inachosha kila siku kupost
#OFF_TO_MWANZA#HEADIN_MBEYA#Oiii on ma way to#Arusha
Mnafikiria hatupendi na sisi kuandika
#LONDON_GET_READY_TONIGHT
#BERLIN_HERE_ICOME
#NIGERIA_SEE_U_SOON
sijui kuna #kizuizi gani hapa katikati!!
Nway inshallah bana…….”

Post a Comment

 
Top