0
Kipindi cha Maskani cha 100.5 Times Fm kinachoongozwa na Gardner G. Habash na DJ Cobo kimetimiza miaka miwili tangu kilipoanza kwenda hewani September 3, 2012.
Kwa mujibu wa meneja wa vipindi wa kituo hicho cha radio, Hermes Joachim maarufu kama Hermy B, kipindi hicho kimepata mafanikio makubwa ambayo ameyapa asilimia 80 ya malengo yao.

Gardner G. Habash na DJ Cobo wakiwa studio
“Kiukweli kimalengo siwezi kusema kwamba nimevuka by 100% hapana.  Lakini naweza kusema kwamba nimefanikiwa by 80%, 20% naiacha kutokana na kwamba huwa kuna ups and downs katika shughuli.” Amesema Hermes.
“Lakini tumefanikiwa kuweza kuraise discussions tofauti tofauti ambazo zinafanya hata baadhi ya vyombo vya habari vingine zinatumia hizo discussion zetu kuripoti taarifa. Na taarifa nyingine zinaibukia ndani ya Maskani yetu ambazo zinakuja kuwa taarifa katika vyombo vya habari vingine. Unakuta hata mwananchi alikuwa hatambui baadhi ya vitu na yeye anafunguka macho.” Amefafanua.
Ameongeza kuwa bado wanahitaji sana sapport kutoka kwa wananchi katika kushiriki kutoa mawazo yao kwa ajili ya kuwajuza watu wengine na pia kusikiliza mawazo ya watu wengine na habari katika kipindi hicho.
Hermes ameeleza wazo na mantiki hasa ya kipindi cha Maskani ilivyozaliwa.
“Unakuta mtu akitoka ofisini, kutokana na mambo mengi…foleni au nini. Unakuta wengi tunatafuta Maskani tunakaa na washitaji zako mnakutana pale, either mnagonga moja mbili au mnakunywa kahawa, mnacheza draft…chochote kile ambacho kinachowaburudisha…mnapiga story. Mnashare ideas za mambo ambayo yamewakuta siku ile.
Sasa tukasema okay…katika muda ule ina maana watu wengi wakitoka (ofisini) kunakuwa labda na foleni nyingi. Kwa nini tusifanye watu wengi ambao wako kwenye magari na sehemu nyingine majumbani ambao hawapo kwenye maskani tukawapa yale ambayo unaweza ukayapata kwenye Maskani. Kwa sababu sio Makani zote ambazo zinaenda kuongelea mambo yasiyo na maana. Kuna maskani nyingine ukienda pale unakutana na watu wazima wenye akili zao na hata vijana ambao wanajitambua na unaweza kupata vitu tofauti tofauti. Kuna mambo ambayo huyajui kabisa kimaisha. Unakuta mwenzako anayajua kwa hiyo unafika pale unafunguka kichwa
“Basically tulikuwa tunataka kufungua milango ya discussions tofauti tofauti ambazo zinakuwa zinazungumzwa na watu tofauti ambao wanakuwa wamekaa pamoja. Na ndio maana ukiangalia Maskani kuna segments, General Knowledge, Open Mic…hivyo ni vitu ambavyo unavipata kwenye Maskani ya kila siku.”
Kipindi cha Maskani cha 100.5 Times Fm, kinakuwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa kumi kamili jioni hadi saa moja kamili. Unaweza kusikiliza kupitia tovuti hii, bofya sehemu iliyoandikwa ‘Listen’.

Post a Comment

 
Top