Bella amesema wimbo huo hauna muda mrefu tangu utoke lakini mrejesho anaoupata kutoka kwa watu wa rika mbalimbali duniani kote unamshangaza. “Nani Kama Mama wiki moja tu ilitoboa vibaya mno, Tanzania nzima mpaka Ulaya,” amesema muimbaji huyo.
“Waafrika kibao ambao wanafuatilia muziki wa Afrika Mashariki, kila siku Napata email, Napata message wanaongelea sana wimbo ‘Nani Kama Mama’. Huu wimbo ni mkubwa sana, nauheshimu sana huu wimbo, ni wimbo mkubwa wa ujumbe na melody. Ni wimbo mkubwa sana ambao umenitengeneza mazingira mengine.”
“Nimeongeza mashabiki wengi sana kwa upande wa Bongo Flava, kwa upande wa bendi, kwa upande wa Taarab. Watu wamezidi kunipenda na kuelewa kazi zangu,” ameongeza.
Post a Comment