Imran Khan na wafuasi wake
Mwanasiasa mashahuri wa upinzani
nchini Pakistan Imran Khan amemtaka waziri mkuu Nawaz Shariff Kujiuzulu
akimshtumu kwa kufanya udanganyifu wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.
Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake katika mji
mkuu wa Islamabad ,bwana Khan amesema kuwa wataandamana katika barabara
kuu za mji huo hadi pale kiongozi huyo atakapojiuzulu.Viongozi hao wawili waliongoza maandamano kutoka mji wa mashariki wa Lahore.
Serikali imesema kuwa iko tayari kuchunguza madai ya udanganyifu ,lakini bwana Sharrif hawezi kuondolewa kupitia mkutano wa hadhara.
Waandishi wanasema kwa maandamano hayo ni changamoto kubwa kwa serikali ya mwaka mmoja ya bwana Shariff.
Post a Comment