magari ya deraya huko Ukraine
Umoja wa mataifa umeonya juu ya
hali mbaya ya kukosekana misaada ya kibinadamu huko mashariki ya
Ukraine, ambako mapigano kati ya vikosi vya serikali na vile vya waasi
waliosambaratika yakiendelea.
katika mkutano wa dharula wa baraza la usalama
la umoja wa mataifa,mkuu wa kitengo cha misaada ya kibinadamu,John Ging,
amesema kwamba bila ya kupatikana kwa suluhu ya kisiasa huko Ukraine
mapigano hayo yatasababisha watu kuwa hatarini zaidi na idadi ya watu
waliokufa kutokana na mapigano hayo itaongezeka.Naye balozi wa Urusi katika umoja wa mataifa,Vitaly Churkin,ameyashutumu majeshi ya Ukraine kwa kuzidisha mashambulizi na kuongeza kwamba raia wapatao elfu nane wa Ukraine wameikimbia nchi yao na kutafuta usalama huko Urusi tangu mapigano hayo yalipoanza.
Post a Comment