Mwalimu mkuu shule ya msingi kamanga Bw.Lucas Nicolaus(Pichani) iliyoko wilaya ya chato amekabidhiwa zawadi ya kinyago cha kutisha (kina sura ya mtu zoba /mburura) baada ya shule yake kuburuza mkia katika matokeo ya mtihani wa taifa (NECTA) wa darasa la saba 2013. Wilaya ya chato huwa na utaratibu wa kuwatunuku zawadi za ngao fedha taslimu kwa shule zilizofanya vizuri na kinyago cha kuogofya kwa shule zilizofanya vibaya. Zawadi hizo ziliztolewa na afisa elimu wa wilaya ya chato Bw.Angasirin Obed Kweka mbele ya baraza la Madiwani wilaya ya chato hapo jana
Mimi nimependa sana utaratibu huu wa kuwatunuku, rai yangu ni kuomba na halmashauri zingine nchini ziige utaratibu huu katika mitihani yote kuanzia shule ya msingi mpaka kidato cha sita,pia na NECTA waige mfano za mtindo huu. wadau manionaje huu mtindo kwani elimu hata ya zile shule kongwe nchini imekuwa ikizidi kushuka siku hadi siku. hii inaweza kuwa njia ya kurudisha hadhi ya elimu yetu kwa kiasi falani.
N.B: Hakuna kuruHUsu kutuma mwakilishi kwenye kupokea zawadi.. mlengwa anatakiwa awe mkuu (kama chato walivyofanya) , makamu au mtaaluma wa shule husika. hii itasaidia kuweka mkazo kwa wasimamizi wa elimu kuwa makini na kazi yao kwa kiasi flani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment