Harry Belafonte akiimba
Muigizaji maarufu na mwimbaji wa
nyimbo ambaye ni Mmarekani Harry Belafonte anatarajiwa kutunukiwa tuzo
ya heshima ya Academy of Motion Pictures Arts and Sciences.
Harry mwenye umri wa miaka 87 pia atapokuea tuzo
ya huduma za jamii kwa kazi zake kama mwanaharakati wa kupinga ubaguzi
wa rangi na masuala ya usawa.Na tuzo hizo zitatolewa pia Tuzo hizo zitatolea mwezi November wakati wa uwasilishaji wa tuzo za Governors.
Harry anajulikana pia kama mfalme wa Calypso, Belafonte ametumia muda wa maisha yake yote akifanya kampeni katika masuala mbalimbali ikiwemo nafuu ya mishara kwa wafanya kazi wa migodini,masuala ya elimu, ufahamu wa ugonjwa wa ukimwi na pia haki za raia.
Belafonte anatajwa kua ni mmoja wa waanzilishi wa harakati za haki za raia na hata kuandaa maandamano ya kudai haki hizo akiwa na hayati Martin Luther King Jr. kutokana na hayo BelfonteHe aliteuliwa kua Goodwill Ambassador wa Unicef mwaka 1987.
Chuo hicho pia kimetaja kazi kadhaa za Belafonte ikiwemo filamu ya kama filamu ya Carmen Jones, Odds Against Tomorrow na The World, the Flesh and the Devil ambazo zilijaribu walau kuonesha kugusia masuala ya ubaguzi wa rangi na uvunjifu wa haki za raia.
Post a Comment