Majeshi ya Ukraine yameuzunguka mji wa Donetski
Afisa mkuu wa umoja wa Ulaya EU
Jose Manuel Barroso amemtahadharisha rais wa Urusi Vladimir Putin
dhidi ya kutuma majeshi yake nchini ukraine kwa kisingizio chochote
kile.
Mazungumzo hayo yalifuatia tangazo la Kremlin
kuwa inapanga mikakati ya kutuma misaada ya kibinidamu mashariki mwa
Ukraine kwa ushirikiano na shirika la Msalaba mwekundu.Msalaba mwekundu haujatoa taarifa ya aina yeyote hadi kufikia sasa.
Takriban watu 1,500 wameuawa baada ya serikali ya Kiev kutuma majeshi yake mashariki mwa taifa hilo katika miji ya Donetsk na Luhansk ili kukabiliana na waasi wanaounga mkono kujiunga na Urusi.
EU yaonya Urusi isiingie Ukraine kwa kisingizio cha kuingiza msaada wa kibinadamu
Duru zinaarifu kuwa majeshi ya Ukraine yamezunguka mji wa Donetsk, mji wenye zaidi ya wakaazi milioni moja na ambao katika siku za hivi punde umekuwa bila umeme na bidhaa muhimu kama chakula na madawa.
Haijajulikana hadi sasa msaada huo na msafara utaondoka lini kuingia Ukraine.
EU imeionya urusi isiingilie kati Mashariki mwa Ukraine
Bwana Barroso alizungumza na rais wa Ukraine Petro Poroshenko ilikujadili hali halisi katika mji wa Luhansk.
Post a Comment