Daktari aliyemtibu mgonjwa wa Ebola ameabukizwa nchini Nigeria
Daktari mmoja jiji Lagos Nigeria amepatikana ameambukizwa na maradhi ya homa ya Ebola.
Daktari huyo ambaye alimtibu mfanyikazi wa
wizara ya hazina nchini Liberia aliyepatikana na homa hiyo ya Ebola na
kuwa mtu wa kwanza kuaga dunia nchini Nigeria sasa amedhibitishwa
kuambukizwa .Waziri wa afya nchini humo Onyebuchi Chukwu amesema kuwa daktari huyo pamoja na watu wengine 70 waliokutana na marehemu wametengwa kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
Mataifa yaliyoathirika na homa ya Ebola
Mlipuko huu wa ugonjwa wa ebola katika ukanda wa magharibi mwa Afrika umesababisha vifo vya watu zaidi ya 826 katika mataifa ya Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Post a Comment