Tuzo alipewa Zanoli
Raia mmoja wa Uholanzi aliyepewa
tuzo na Israel kwa kumficha mtoto mmoja wa kiyahudi wakati wa vita vya
dunia vya pili amerudisha medali aliyopewa baada ya ndege moja ya
kijeshi ya Israel kuiharibu nyumba ya wakwe wa mpwa wake mkubwa.
Watu sita wa familia hiyo waliuawa.Henk zanoli ambaye ana umri wa miaka 91 na mamaake walipewa tuzi hiyo inayopewa watu wasio wayahudi ambao hueka maisha yao hatarini kuwalinda wayahudi kutoka kwa watu Wa Nazi.
Bwana Zanoli ameliambia gazeti la Haaretz kwamba kwa kuhifadhi tuzo hiyo itakuwa ni kuwatusi watu wa familia hiyo waliouawa katika eneo la Gaza.
Post a Comment