zaidi ya watu milioni moja wa sudani kusini wamekimbia mapigano
Takriban watu milioni nne nchini
Sudani kusini wako hatarini kukabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula
mwezi ujao, Mashirika ya misaada ya Uingereza yametaadharisha.
Zaidi ya Watu milioni moja wamekimbia makazi yao
baada ya kuibuka mapigano mwezi Desemba mwaka jana kati ya makundi
yanayokinzana ya Chama kinachotawala nchini humo.Maelfu ya watu wamepoteza maisha kutokana na mgogoro ulioanza kama mgogoro wa kisiasa kati ya Rais wa Sudani kusini, Salva Kiir na aliyekua makamu wake,Riek Machar.
Kamati inayoshughulikia majanga ambayo inashirikiana na mashirika 13 ya misaada kutoka Uingereza ambayo hushughulikia majanga kimataifa,imesema inapungukiwa fedha kwa kiasi ya chini ya asilimia hamsini ya fedha zinazohitajika ili kupambana na tatizo la upungufu wa chakula nchini Sudani kusini.
Wataalam wa kimataifa wa maswala ya chakula wanasema kuwa iwapo mzozo utaendelea nchini humo na iwapo hawatapata misaada Zaidi, maeneo mengi ya Sudani kusini yatakumbwa na janga la njaa ifikapo mwezi Agosti.
Post a Comment