Mazishi ya kijana wa kipalestina aliyetekwa nyara na
kuuawa mjini Jerusalem yameahirishwa kutokana na mgogoro kuhusu siku
mwili wa kijana huo utakapokabidhiwa kwa familia.
Familia ya Mohammed Abu Khdair imesema Polisi wamekataa kuwapatia mwili huo, madai ambayo polisi imekanusha.Israel ilitekeleza mashambulizi ya anga katika eneo la Gaza siku ya alhamisi dhidi ya wanamgambo.
Maafisa wa Israel wamesema wanamgambo walitekeleza mashambulizi ya roketi tangu asubuhi siku ya jumatano na kuharibu nyumba lakini hakuna aliyejeruhiwa.
Maafisa kutoka Wizara ya afya ya Gaza wameiambia BBC kuwa wapalestina 10 walijeruhiwa katika shambulio la anga na kukimbizwa hospitalini.
Post a Comment