Watu kadhaa katika mji wa Dille,
Kaskazini mashariki mwa Nigeria, wameuawa, na wengine kutorokea vijiji
jirani baada ya kushambuliwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa
Boko Haram.
Aidha, nyumba kadhaa zilichomwa katika shambulizi hilo lililotekelezwa siku ya JumatatuAnavyoripoti Raliya Zubairu kutoka Abuja, viongozi nchini Nigeria wamedhibitisha shambulizi hilo, lakini hawajatoa usemi ni watu wangapi waliuawa.
Hata hivyo wanapeleleza madai ya raia kuwa walishambuliwa na ndege za wanajeshi.
Shahidi aliyezungumza na BBC alisema watu 25 waliuwawa, huku wanamgambo 20 wakiuawa na wakaazi wanaoshika doria katika eneo hilo.
Hayo yakijiri, wanaharakati wa haki za kibinadamu wametoa ripoti hii leo inayosema kuwa takriban watu elfu mbili wameuwawa na wanajeshi tangu mwanzoni mwa huu mwaka.
Post a Comment