Uuzaji wa tiketi za Madola wasimamishwa
Waandalizi wa mashindano ya
jumuia ya madola mwaka 2014 huko Glasgow wamefunga mtandao wake wa kuuza
tiketi ili kutanzua kwanza tatizo lililopo la uuzaji tiketi.
Glasgow 2014 inasema kuwa tahadhari hiyo ni bora
ili kuangazia maswala tata yanayotatiza uuzaji wa tiketi zingine za
ziada zipatazo elfu kumi tangu siku ya jumatatu juma hili.
Uuzaji wa Tiketi za Madola waahirishwa
Uuuzaji wa tiketi mtandaoni kwa mara ya kwanza ulianza rasmi jumatatu wiki hii.
Umaarufu wake kupitia mitandao ya kijamii ulisababisha kununuliwa kwa kasi huku wauzaji wakashindwa na ununuzi huo mkubwa na wa haraka.
Watu wengi wanasema kuwa wamekuwa wakijaribu kununua tiketi kwa kipindi cha masaa 24 mtawalia.
Aidha kunao walio lalamikia matatizo ya simu katika uagizaji wa tiketi hizo.
Post a Comment