Stori: Mwandishi Wetu, Dodoma
SAKATA la
mawaziri kutajwa kuwa ni mizigo, lililoibuliwa kwa mara ya kwanza na
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye,
limeibuka tena mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha viongozi hao
kujipanga ili kujitetea, ndani na nje ya Bunge la Bajeti linaloendelea
mjini Dodoma.
Wakati Nape alirudia kauli yake hiyo kwa mara nyingine wiki iliyopita
mjini Igunga, Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola naye alimwita Waziri wa
Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza kuwa ni mzigo kwa kitendo
chake cha kushindwa kuwajibika, hasa katika sakata la mbegu za pamba.
Habari kutoka kwa watu walio karibu na mawaziri wanaotajwa kuwa ni
mizigo, zinasema ili kuhakikisha hawapati shinikizo kama ilivyokuwa mara
ya kwanza, wamejipanga kujitetea kwa nguvu zote, ndani na nje ya Bunge,
kwa kigezo kuwa wanaopiga kelele dhidi yao, wanatumiwa na wapinzani wao
kisiasa majimboni.
“Hali siyo nzuri kabisa kaka, wameshtukia kuwa kuna njama za makusudi
za kuwang’oa, wanataka kutumia hii nafasi kujinasua, kwa hiyo kuna
mikakati inapangwa kuonyesha kuwa kelele dhidi yao zina mkono wa
wapinzani wao kisiasa, wanadai hata wanaopiga kelele kutoka CCM, nao
wanatumiwa,” kilisema chanzo hicho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment