Maeneo ya Mwabepande yanavyoendelea kuchakaa kama yanavyoo onekana. Picha na Kalunde Jamal.
Dar es Salaam. Anaendelea kusimulia kuwa baada ya kuapata somo
hilo mwanae akasema wasome dua kila mmoja ya kwake wakimshirikisha na
baba yake, kwa kuwa hali ilikuwa ni ya hatari na maji ni mengi na
yalikuwa yanazidi kujaa. “Tukasoma dua na kila baba yake alipokuwa
akituhimiza kuondoka, kijana alisisitiza tuendelee kusoma akiamini hata
kama tukifa kila mmoja afe akiwa salama,” anasema.
Zainabu anaongeza kuwa baada ya dua walijitosa
majini na kufanya kama alivyoambiwa kwa bahati nzuri walifika salama
nchi kavu, lakini kijana wake alimzia mara kadhaa.
“Cha kushangaza baada ya kufika nchi kavu kijana
wangu alianza kuzimia mara kadhaa, kila akizinduka anazimia tena, lakini
akapatiwa huduma ya kwanza na baada ya kurudi kwenye hali ya kawaida
akasema haamini kama ameniokoa na hata alipokuwa akiniokoa hakuwa yeye
bali ni bua, kwani alikuwa amekata tamaa ya maisha yao tena,” anasema
Zainabu huku akisema kisa hicho ndiyo kinamfanya avumilie lolote
linalotokea katika jangwa hilo.
Anasema kuwa kamwe hawezi kurudi kule tena na
kuiomba Serikali kuwafikiria na kulifanyia kazi suala lao mapema kama
alivyoagiza Rais.
Wakazi wengine wanaizungumziaje hali hiyo
Hashimu Saidi ni moja ya wakazi waliopata hifadhi
katika eneo hili anasema kuwa alipopata matatizo na kuhamia katika eneo
hilo, alikuwa na familia yake ambayo ilikuwa ni mkewe na wanawe wawili,
lakini amelazimika kumrudisha mkewe kwao Lindi kutokna na hali kuwa
ngumu.
Anasema wakati wanafika eneo hilo mwaka jana
kulikuwa na mvua wakapewa mahema ambayo waliambiwa yanadumu kwa miezi
sita hadi nane, lakini sasa ni zaidi ya mwaka bado wanaishi katika
mahema hayo ambayo kwa sasa hayafai tena.
“Kipindi tunakuja huku kulikuwa na mvua za msimu
huu zimenyesha, tena yameraruka na limekuwa siyo eneo salama la kuishi
kwa kuwa hali ni mbaya upepo kama unavyoona,” anasema Saidi na kuongeza
kuwa:
“Nikiona kipande cha bati hata kama ni mbali vipi
naokota, nikiona boksi naokota kila ambacho naamini kitanisaidia kuziba
hema hili naokota, ndiyo maana nimemudu kuwa hapa hadi leo lakini hali
ni mbaya sana,” analalamika Saidi.
Aidha, Saidi anasema kuwa kibaya zaidi waliahidiwa
kupata mifuko 100 ya sementi kutoka kwa Rais na mabati 30, ambayo
ilikuwa ni ahadi ya mmiliki wa Kampuni ya Home Shopping Center ambayo
aliitoa mbele ya Rais alipowatembelea, lakini cha kushangaza hadi sasa
hakuna kinachoendelea na hawajui wamuulize nani.
Anaendelea kulalamika kuwa hata viongozi waliokuwa
wakifika eneo hilo kwa ajili ya kuwapa taarifa hizi na zile sawa
hawafiki tena, licha ya Rais kutoa angalizo wabadilishiwe mahema na
Chama cha Msalaba Mwekundu hivyo nacho hadi sasa hakijafanyika.
Mwananchi ilimtafuta Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
, Said Meck Sadiki, amelitolea ufafanuzi suala la sarujiambalo Rais
aliagiza wakazi hao wapewe, kwa kusema kuwa mchakato unaendelea lakini
unafuata sheria za ununuzi wa Serikali na ndiyo maana unachukua muda
mrefu kukamilika.
Alisema kuwa fedha za Serikali hazitoki kama njugu au pipi kama
wanavyotaka wakazi wa maeneo hayo, bali zinahitaji mipangilio maalumu
ikiwamo kufuata sheria na utaratibu uliowekwa.
Mkuu huyo pia alizungumzia uamuzi uliochukuliwa na
wakazi wa eneo hilo kurudi katika maeneo yao ya awali, kwa madai kuwa
mahema waliyopewa yamekwisha na hakuna utaratibu mwingine wa kupewa
mapya, kuwa hakuna mpango wa kupewa mengine na hiyo ipo duniani kote
kuwa msaada unakuwa ni kwa mara ya kwanza na wala siyo siku zote kama
wanavyodhani wao.
“Ule ulikuwa ni msaada wa ghafla na kizuri zaidi
na maeneo wamepewa kwa muda wote huu wameshindwa kujenga hata vibanda
imara vya kuishi wanasubiri mahema mengine watayapata wapi hakuna mpango
huo”alisema Sadiki.
Aidha Sadiki alitoa ufafanuzi kuhusu wakazi wa
eneo hilo waliorudi mabondeni, kuwa shauri yao hakuna atakayewafunga
kamba na yatakapotokea mafuriko wasitegemee kupata msaada tena, kwa kuwa
wameamua wenyewe kwa makusudi kurudi sehemu ambayo si salama.
“Tuliwasaidia kwa kuwa hawakuwa na pa kwenda na
hakukuwa na utaratibu wa kuwahamisha kule hapo kabla lakini sasa eneo
lipo na kila mmoja amepewa la kwake, sasa kama yupo aliyerudi kwa hiyari
yake akidhani anaikomoa Serikali shauri yake, hatuwezi kuwafunga kamba
au kubembeleza warudi,” alisema Sadiki.
Post a Comment