SHEHE PONDA: AFUNDISHA WAFUASI WAKE KUJITOA MHANGA ? YADAIWA NDIO WANAOFANYA MASHAMBULIZI YA ACID ZANZIBAR, AJIPANGA KUGOMBEA URAIS
Katika kile kinachoonekana dhahiri serikali kushindwa kuchukulia hatua Shehe Ponda na wafuasi wake wameendelea kua mwiba mkali kwa Tanzania na mataifa ya nje baada ya kusemekana kua wafuasi wa shehe huyo ndio wanaoongoza mashambulizi ya kumwagia watu acid katika visiwa vya Zanzibar.Katika uchunguzi uliofanywa na jipange101 umebaini kua shehe huyo anatoa mafunzo ambayo hatukuweza kujua yanahusiana na nini hasa na pia baadhi ya wakazi waliofanya mahojiano nasi hawakuweza kubainisha ni mafunzo ya nini kwani hutolewa katika usiri mkubwa. “Nafahamu kuna watu anawafundisha lakini sijui hasa atakua anawafundisha mafundisho gani kwasababu mafundisho ya Dini yetu ya kiislamu sio ya siri hivo” Alisema kijana aliefahamika kwa jina la Omari (Unguja).
Hivi karibuni serikali ya Tanzania imeonekana kushindwa kudhibiti hali ya kushambuliwa kwa wageni na wenyeji wanaotoka upande wa pili (yaani Tanganyika) kwani mashambulio mengi hua yanajirudia zaidi ya mara moja.
Mabinti 2 wa Kiingereza walishambuliwa mara ya kwanza na binti wa kiislamu huku sababu ikitajwa kua kufanya jambo lisiloruhusiwa kufanywa katika kipindi cha mfungo,mabinti hao hao 2 walishambuliwa tena kwa kumwagiwa tindikali (acid) ndipo vyombo husika vikashtuka na kuanza kufuatilia.
“Haya mashambulizi serikali inajua sana kwani mengine yanapangwa kushirikiana na Polisi wenyewe ama baadhi ya viongozi kwa maslahi yao,kwani nani aisejua uamsho wannashambulia watu na kufanya fujo? ama yule shehe Ponda nani asiemjua hapa Unguja kua anakikundi cha fujo ?” “Usituone hivi hapa hata kutembea sisi wenyewe wakati mwingine twaogopa,ushanifahamu” Alisema binti aliejiambulisha kwa jina la Zainabu (Pemba).
Hivi karibuni vyombo vya habari na tovuti mbalimbali vilitangaza nia ya shehe huyo kugombea Urais wa Zanzibar/Tanzania.Shehe huyu anaeshinikiza utawala wa kiislamu na kuvunjika kwa Muungano amekua akisumbua vichwa vyombo vya usalama kwa kile kinachodhaniwa kua na mtandao mkubwa mpaka ndani ya vyombo hivyo kiasi cha kushindwa kumdhibiti inavyotakiwa.
“Mimi nashangaa kwa nini serikali inamshindwa mtu kama huyu, kwani rais hakumbuki waliokua wasumbufu kipindi cha Mwalimu walifanywa nini? walifungiwa kijijini kwao na kunyimwa haki zote za kusafiriwa na kufutiwa vyeti vyote ama wengine waliuliwa kimya kimya,ama kupewa kazi nje ya nchi,kuna njia nyingi mbona za kutuliza watu kama hao ama kwa sababu muislam mwenzie,ni upuuzi tu mimi hainiingii wanamshindwaje huyu mtu” Alilalamika kijana aliejitambulisha kwa jina la Juma (Dar Es Salaam).
Inaonekana kuna mambo makubwa na mipango isiyofahamika nia yake ni nini hasa inayoendelea kupangwa na Shehe huyu lakini katika vitu ambavyo vinazungumzwa nan wengi ni kua amekua kinara kupinga Muungano wa Zanzibar na Tanganyika tangu atoke kizuizini,na anapinga Muungano wa vyama vya siasa kati ya CCM na CUF huko Zanzibar na kutaka Zanzibar iunganie na nchi za Kiislam zenye msimamo mkali.
Post a Comment