0


Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Assah Mwambene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa News for Rwanda na wanyarwanda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana.
Advertisement

Thumbnail for 13763
“Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,”amesema Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.
Madai hayo yaliandikwa jana na mitandao ya Rwanda wakidai kuwa mama Salma Kikwete ni Mnyarwanda na ni binamu wa aliyekuwa rais wa zamani wa Rwanda.
Wakati huo huo, wadadisi wa mambo wa kimataifa wameonesha kushangazwa na hatua ya makusidi ya Wanyarwanda ya kujaribu kumpakazia Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete, Mmakonde wa Lindi, kwa kumzushia mambo ya ajabu. 

Post a Comment

 
Top