Home
»
KITAIFA
» Askari Polisi wa kituo cha Oysterbay mbaroni kwa ujambazi
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limewatia mbaroni
majambazi tisa wa kutumia silaha akiwemo askari polisi wa kituo cha
polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaamu Bw. Suleimani Kova
amesema majambazi hao wamekamatwa katika operesheni maalum ya jeshi hilo
ambapo pia walifanikiwa kukamata sare za jeshi la wananchi Tanzania
(JWTZ) zinazoaminika kutumika katika uhalifu pamoja na silaha na risasi.
Aidha kamanda kova ameeleza kukamata magari yanayosadikika kutumika
katika uhalifu tofauti pamoja na yenye namba za usajili T865CEH aina ya
Carina, na T967 AUG carina.
CHANZO: ITV
Post a Comment