Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wamekusanyika katika
mgodi mkubwa wa dhahabu nyeupe kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuuawa kwa
wachimba migozi 34. Chama tawala cha ANC kimesema hakitahudhuria
makumbusho ya leo kikisenya yanatumiwa kukejeli utawala wa nchi.
Katika maadhimisho hayo Afisa mtendaji wa
kampuni ya, Lonmin, Ben Magara amwaomba mshamaha familia za wachimba
migodi 34 waliouawa. AMCU ndicho kikubwa zaidi katika mgodi wa dhahabu nyeupe inayomilikiwa na kampuni ya Lonmin.Baadhi katika chama tawala cha ANC wameelezea hofu huenda chama hicho kikaungana na aliyekua kiongozi wa vijana Julius Malema ambaye alifukuzwa chamani kwa makosa ya nidhamu.
Malema ameunda chama chake cha kisiasa. Rais Jacob Zuma aliunda tume ya kuchuguza matukio yaliyopelekea mauaji ya wachimba migodi hio. Mwandishi wa BBC Afrika Kusini anasema kumekuwa na ghathabu ya umma kwani hadi sasa hakuna polisi hata mmoja aliyewajibishwa na mauaji hayo.
Post a Comment