0


MPENZI msomaji, bado naendelea kuelezea mambo kumi yanayosababisha mwanamke kusaliti. Usichoke, endelea kuwa sambamba nami hadi mwisho naamini utapata darasa la kutosha.
Wiki iliyopita nilieleza kwamba mwanaume kutuama kifuani kwa muda mrefu ukidhani atakuona kijogoo unachelewa kufika mwisho, unajidanganya. Zaidi atakuona msumbufu usiyejua mapenzi.
Epuka sana hilo, kuhakikisha hilo halitokei ni kufanya juu chini katika kuziweka hai hisia zake.
Usipande naye kitandani kama hayuko tayari.
Vilevile kama umejiridhisha yupo tayari, hakikisha unapopanda naye kitandani mnashuka akiwa ameridhika kwa kiwango cha kutosha. Usimuache na hali ya manung’uniko ya kwamba hajatosheka. Ukiiruhusu hali ya aina hiyo, unakuwa unajitafutia majanga kwenye uhusiano wako.
Mmepanda kitandani, hebu ruhusu mazungumzo mepesi yenye maswali ya hapa na pale yachukue nafasi ili kila mmoja ajue nafasi ya mwenzake wakati wa tendo. Mkienenda kama mabubu, hamtahusika kikamilifu. Itakuwa sawa na mbuzi ambao kwao suala la hisia halijadiliwi kabisa. Beberu anapotaka anapanda na anapomaliza anashuka.
Penda kuuliza nafasi yake wakati wa tendo, namna anavyopokea huduma na ujibidishe kumfikisha kileleni. Kinyume na hapo, atakuona mtu usiye na jipya kwake. Ni binadamu, kwa hiyo yanapomzidi atatafuta mbadala wako atakayeweza kumpeleka kule anapopataka.
6. KUHISI YUPO KWENYE UHUSIANO WA SHERIA NA AMRI
 Kwa kawaida wanawake hawapendi kuamrishwa wala kuwekewa sheria. Asili yao ni viumbe dhaifu, kwa hiyo hupenda wawe wanaishi kwa kufanya makosa na wanaume wao wawaelewe na kuwachukulia hivyohivyo. Hata kuambiwa, hutaka waambiwe kwa lugha nyepesi, isiyo na ukali.
Inapotokea anafanya kosa halafu anakaripiwa kwa nguvu, huanza kuuona uhusiano ni mchungu. Humuona mwanaume wake ni mtu mwenye hasira, kwa hiyo moja kwa moja humtoa kasoro katika sekta ya mapenzi. Wanawake hupendelea zaidi kuwa na wanaume laini.
Hupendelea kuona kwamba hata kama ana makosa lakini asikose ujasiri wa kumsogelea mwenzi wake. Inapotokea mwanaume wake ni mtu mwenye maswali mengi na hodari wa kupaza sauti kumgombeza, huanza kumwogopa na baadaye kujiona yupo kwenye uhusiano ambao hana uhuru nao.
Maneno kama “Lazima”, “Nimesema”, “Ole wako” na mengineyo yenye tafsiri sawa na hayo, anapoambiwa mwanamke, moja kwa moja huhisi anageuzwa mtumwa wa mapenzi. Atajiona ananyanyaswa, kwa hiyo atataka ukombozi. Jinsi anavyojikomboa ndivyo anavyosaliti.
Ile hali ya kujihisi hayupo huru kwenye uhusiano wake, namna anavyohisi ananyanyasika, humfanya akose raha na msisimko wa mapenzi. Sasa basi, kwa vile anahitaji raha na msisimko, ndipo hujikuta anadondokea kwa mwanaume wa pembeni ambaye atakuwa karibu naye, anayeonesha dalili njema za kimapenzi.
Itaendelea wiki ijayo.

Post a Comment

 
Top