Wakimbiaji wa kwanza katika mbio
za London wameshamaliza na Priscah Jeptoo wa Kenya ameshinda mbio za
wanawake na raia wa Ethiopia, Tsegaye Kebede, ametokea wa kwanza upande
wa wanaume.
Ulinzi ulikuwa mkubwa lakini hakuna ripoti za kutokea lolote.
Watu waliokufa Boston walikumbukwa mjini London kwa watu kukaa kimya kwa sekunde 30 kabla ya mashindano kuanza, na wakimbiaji waliombwa wavae kitambaa cheusi.
Watu zaidi ya 30,000 walishiriki kwenye mashindano hayo na malaki walishangilia kando ya mabarabara.
Post a Comment