0
MKAZI wa kijiji cha Ndanga wilayani Kyela mkoani Mbeya, Edward Mwakalebela (86), ambaye ni mganga wa tiba za jadi, anatuhumiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka sita (jina tunalo). Akizungumza na MTANZANIA jana, mama mzazi wa mtoto huyo, Sioni Ijuni, alisema tukio hilo lilitokea juzi. Alisema mtoto huyo, alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo na ndipo mama yake aliamua kumpa huduma ya kwanza kwa kumkanda na maji ya moto.

Alisema baada ya kumkanda, ghafla alianza kuona damu zikitoka sehemu za siri.

Alisema alipomhoji mtoto huyo, alimtaja babu huyo kuwa alimuingilia kimwili na kumfanyia kitendo hicho cha kinyama.

Mzee huyo, ambaye wanaishi jirani, alikuwa na mazoea ya kumtuma mtoto mara kwa mara kama vile mjukuu wake.

Kutokana na hali hiyo, mama huyo aliamua kupeleka taarifa kwa mwenyekiti wa kijiji, akiwa na mume wake, Kifoji Mwabusila, ambaye walitengana na wanaishi mbalimbali.

Alisema walipofika kituo cha Polisi, walipewa kibali kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu katika hospitalini ya wilaya ya Kyela na polisi kwenda kumkamata mtuhumiwa na kumtia hatiani.

“Tulipokuwa kwa mwenyekiti wa kijiji, babu huyo alikiri kutenda kosa hilo na aliomba msamaha akidai ni shetani tu alimpitia, huku akiomba mambo hayo yamalizwe kimya kimya bila kwenda polisi, jambo ambalo lilikuwa gumu kwetu kulikubali,” alisema.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Dickson Mwakasinga, alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kuwa baada ya kuletewa taarifa, alifuata taratibu zote na kumkabidhi mtuhumiwa huyo mikononi mwa polisi wilaya kwa hatua zaidi za kisheria.

Kwa upande wake, mganga Tabu Mwakalundwa alikiri kumpokea mgonjwa huyo na kudai kuwa mtoto huyo aliingiliwa na kuharibiwa vibaya.

Post a Comment

 
Top