Madhila baado yamendelea kwa jamii ya kiislaam nchini Tanzania baada
ya Serikali kibaraka ya nchi hiyo kuja na mkakati na mbinu mpya wa
kupambana na Uislaam wa kupinga watoto wa kiislaam kufundishwa masoma ya
Dini yao.
Habari
kutoka Kanda ya Ziwa Magharibi mwa Tanzania zinaeleza kuwa Maaskari wa
kupambana kwa kile walichokiita Ugaidi walikivamia chuo cha kuhifadhisha
Qur'an kilichopo Ilemela mjini Mwanza siku ya jumamosi uliopita.
Walioshuhudia
wanasema Maaskari hao wakiwa na Silaha zao walikivamia chuo hicho na
kuwatoa baadhi ya vijana waliokuwa na Umri wa miaka 15 hadi 17 na kusema
kuwa hawajafikia umri wa kusomeshwa kuhifadhi Qur'an.
Machi,7
mwaka huu Serikali kibaraka ya nchi hiyo iliwafukuza watoto 17
waliokuwa wakisoma chuo cha kuhifadhisha Qur'an katika mji wa Moshi.
Mkuu
wa Wilaya wa Moshi Novatus Makunga amesema kwa sasa chuo hicho
imefungwa na watoto wote wameondolewa na kurjeshwa kwenda kusoma shule
ambazo huharibu ubongo za watoto wa Kiislaam.
Abdulnasir
Abdurahim ambae ni mwalimu wa chuo hicho amesema chuo inawafundisha
watoto wa Kiislaam kuhifadhi Qur'an tukufu ambayo ni msingi wa Dini yao.
Kati
ya Machi 25 na 27 mwaka huu Maaskari wa kupambana na Uislaam waliingia
kwa nguvu misikiti ya Bilal uliopo mtaa wa kibaoni Wilayani Hai Mkoani
Kilimanjaro na Masjid Othman uliopo Uzunguni na kuwakamata watoto zaidi
ya 147 na kudai kuwa walikuwa wakifundishwa masomo yalio kinyume na
sheria.
Mkuu
wa Wilaya ya Hai Anthony Mataka,amethibitisha kuwepo uvamizi huo wa
Maaskari dhidi ya Misikiti hizo na kuwalaumu waalimu wa wanaofundisha
masomo ya Dini.
"tukio
hiyo lipo na wanaohusika ni watu wanaotumia mwamvuli wa Dini fulani
kufanya mambo yasiofaa katika jamii,kwahiyo naziomba Mamlaka husika
ikiwemo Baraza kuu la Waislaam (Bakwata) kutambua Misikiti na shughuli
zinazoendelea katika nyumba hizo za Ibada,Hili
lazima walifanyie kazi kwa sababu hao vijana inasemekana wanafundishwa
mazoezi makali ya kareti na judo katika nyumba hizo za ibada,” alisema
Mtaka.
Mbinu
huu mpya wa Serikali ya Tanzania ni sehemu ya mkakati vita dhidi
Uislaam inayolenga kuangamiza jamii ya Kiislaam walio wengi katika nchi
hiyo iliyopo katika Bara la Afrika Mashariki.
Post a Comment