Hali ya usalama katika miji mikubwa nchini Kenya umewekwa katika hali
ya tahadhari baada ya shambulio kubwa iliyofanyika katika chuo kikuu
cha Garissa kusababisha hasara Kaskazini Mashariki.
Habari
kutoka mjini Nairobi nchini Kenya zinaeleza kuwa watu zaidi ya 141
wamejeruhiwa baada ya kutokea mkanyagano ndani ya chuo kikuu cha Nairobi
kutokana na hofu ya mashambulio kutoka kwa Al-Shabab.
Katika
hali isiyo ya kawaida ambapo wanafunzi wa chuo hicho walikuwa
wakitegema kutokea shambulio ndani ya chuo hicho baada ya taarifa
kusambazwa kwenye mtandao ambao ulisemekana kusambazwa na watu
wasiojulikana.
Mtu
mmoja amefariki kutokana na mkanyagano hayo ndani ya huo hicho,Benson
Kibue ambae ni Mkuu wa Polisi mjini Nairobi amethibitisha kutokea tukio
hilo na kuongeza kuwa wengi wa waliojeruhiwa walikuwa wakikimbia hovyo
na hitilafu ya umeme kusababisha mlipuko mkubwa ndani ya chuo hicho.
Watu
waliojeruhiwa wamelazwa katika Hospitali ya Kenyatta mjini
Nairobi,Madaktari wamesema waliojeruhiwa wamevujinjika viungo baada ya
kujaribu kuruka kupitia Madirisha ya Jengo la chuo hicho ambao ni
Ghorofa sita na wengine kuongua na moto.
Wiki
mbili zilizopita shambulio iliyotekelezwa na Mujahidina wa Somalia
yalisababsiha vifo vya watu zaidi 170 na mamia kujeruhiwa katika chuo
kikuu cha Garissa.
Post a Comment